Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Mohammad Jawad Zarif ameilaumu Marekani kwa kusema,
"Utawala wa Washington unawajibika kwa vurugu zozote zinazoweza kutokea katika eneo hili,".
Kulingana na taarifa iliyoandikwa na kutolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Zarif alikuwa na mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya nje wa Qatar Muhammed bin Abdurrahman Al Thani na Waziri wa Mambo ya nje wa Armenia Ara Ayvazyan.
Zarif alijadili uhusiano wa nchi mbili na maendeleo ya kikanda na mwenzake wa Qatar.
Akiashiria kwamba nchi katika eneo zinapaswa kuchangia usalama na utulivu bila uingiliaji wa wageni, Zarif aliishutumu Marekani kwa kuchukua hatua "za tuhuma na uovu",
"Utawala wa Washington unawajibika kwa vurugu zozote zinazowezekana katika eneo hili," alisema.
Katika mazungumzo yake ya simu na Waziri wa Mambo ya nje wa Armenia Ayvazyan, Zarif alisema kuwa kumalizika kwa vita huko Karabakh kuliunda msingi wa ushirikiano wa pande nyingi kati ya nchi za eneo hilo.