Saturday, December 12, 2020

DC Jokate alitaka baraza jipya la madiwani lililoapishwa kuvunja makundi

 


MADIWANI wa baraza jipya  la halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani wameonywa na kutakiwa kuvunja kabisa makundi  ya kisiasa ambayo yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu na badala yake wahakikishe wanaungana na kuwa kitu kimoja katika kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi ikiwemo suala la utatuzi wa migogoro ya ardhi pamoja na kujikita zaidi katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo wakati wa halfa ya kuwaapisha madiwani wapatao 23 ambao  kati yao sita ni wa viti maalumu na 17 wa kuchaguliwa na kuwahimiza kuchapa kazi kwa weledi kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo na kuwaondolea kero ambazo zimekuwa zikiwasumbua.


Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Zuberi Kizwezwe asema kwamba kipaumbele chake kikubwa ni kuhakikisha kwamba anashirikiana bega kwa bega  na  madiwani wenzake katika kuboresha sekta ya afya na upatikanaji wa  maji safi na salama   hasa katika maeneo ya vijijini.


Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katika nafasi ya Mwenyekiti alikuwa na haya ya kusema huku Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Mwanana Msumi aliwataka viongozi wote waliochaguliwa kuwataka  kufanya kazi kwa ushirikiano.


BARAZA la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe tayari limeapishwa rasmi ambapo pia limefanya uchaguzi ambapo  Zuberi Kizwezwe amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya kwa kupata kura zote 23 za ndiyo huku nafasi na Makamu mwenyekiti ikienda kwa Mohamed Lubondo kura 23.


KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...