Sunday, December 13, 2020

Adhabu ya kifo yatekelezwa dhidi ya mtu mwingine Marekani



 
Mwanaume aliyemuua binti yake karibu miaka 20 iliyopita amekuwa mfungwa wa pili Marekani kuuawa.

Kifo cha Alfred Bourgeois kwa sindano siku ya Ijumaa kinakuja baada ya Brandon Bernard kuuawa Alhamisi kwa saa za eneo hilo


Hukumu nyingine za kifo dhidi ya watu wengine watatu zimepangwa kabla ya kumalizika kwa urais wa Donald Trump tarehe 20 mwezi Januari.


 
Hukumu ya kifo haikutekelezwa kwa miaka 17 kabla ya Bw Trump kuamuru kuanza tena kwa hukumu hiyo wanzoni mwa mwaka huu.


Ikiwa hukumu iliyobaki dhidi ya watu watatu itaendelea, Bwana Trump atakuwa amesimamia mauaji zaidi kuwahi kufanywa na rais wa Marekani kwa zaidi ya karne moja.

Bwana Biden, ambaye kwa miongo kadhaa alikuwa akiunga mkono kwa nguvu adhabu ya kifo akiwa seneta wa Delaware, sasa amesema atatafuta namna ya kuondosha adhabu ya kifo nchini Marekani mara atakapoanza majukumu yake ya urais.

Adhabu ya kifo nchini Marekani haikutekelezwa tangu mwaka 2003, kwa sehemu kwa sababu ya wasiwasi kuhusu dawa zinazotumiwa wakati wa kunyonga.

Kosa
Mahakama zilisema kwamba Bourgeois alikuwa akimdhalilisha kimwili na kingono binti yake wa miaka miwili kabla ya kumuua alipopita Texas wakati akifanya kazi ya dereva wa lori kwa muda mrefu.

Waendesha mashtaka wanasema alimuua kwa kumpigiza kichwa chake kwenye dirisha la gari na dashibodi baada ya kupindua sufuria yake ya mafunzo kwenye ndani ya gari wakati baba huyo alipokuwa akiliegesha gari hilo.

Bourgeois, ambaye alihukumiwa kifo mnamo 2004, alikuwa akifikisha bidhaa katika kituo cha jeshi wakati alipomuua binti yake kwa hivyo alishtakiwa katika mahakama kuu .

Mawakili wake walisema kwamba alikuwa na matatizo ya kiakili ambao ulipaswa kumzuia kupata adhabu ya kuuawa.

Brandon Bernard aliuawa huko Indiana baada ya ombi la huruma dakika za mwisho kukataliwa na Mahakama kuu ya Marekani.

Bernard, 40, alihukumiwa kwa mauaji mnamo 1999 wakati alikuwa kijana, na ndiye mkosaji mdogo kabisa kuuawa na serikali ya Marekani kwa karibu miaka 70.

Wafungwa wengine wanaotarajiwa kunyongwa
Lisa Montgomery alimnyonga mwanamke mjamzito huko Missouri kabla ya kumkata na kumteka nyara mtoto mwaka 2004. Amepangwa kuuawa tarehe 12 Januari. Mawakili wake wamesema alipata dosari kwenye ubongo kutokana na kupigwa akiwa mtoto na anaugua ugonjwa mbaya wa akili. Atakuwa mwanamke wa kwanza kukabiliwa na hukumu hiyo tangu mwaka 1953.

Cory Johnson alihukumiwa kwa mauaji ya watu saba, kuhusiana na kuhusika kwake na biashara ya dawa za kulevya huko Richmond, Virginia. Timu ya kisheria ya Johnson imesema kuwa ana shida ya kiakili, inayohusiana na unyanyasaji wa mwili na mihemko aliyopitia akiwa mtoto. kifo chake kimepangwa kutekelezwa tarehe 14 Januari.

Dustin John Higgs alihukumiwa baada ya kuhusika na vitendo vya k utekaji nyara na mauaji ya wasichana watatu mnamo mwaka 1996 Washington, DC. Higgs hakuua mwathiriwa wake yeyote, lakini alimwagiza mshtakiwa mwenzake Willis Haynes kufanya hivyo. Haynes amesema katika nyaraka za mahakama kwamba Higgs hakumtishia, au kumlazimisha afyatue risasi. Higgs amepangiwa kunyongwa tarehe 15 Januari.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...