Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wanaofanya mipango ya kuhamasisha maandamano bila kufuata sheria na kusababisha taharuki kwa wananchi sambamba na mipango ya kuharibu mali, miundombinu.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amedai kuwa mpaka sasa wanawashikilia watu 14.
"Tuwamemkamata mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Chadema bwana Freeman Mbowe pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Boniface Jacob na wengine ambao wanatimiza idadi ya watu 14" alisema Mambosasa.
Aliendelea kusema kuwa aliyegombea nafasi ya urais kupitia chama hicho Tundu Lissu, alikamatwa jana na kuachiwa baada ya muda mfupi.
Aidha Kamanda Mambosasa amesema watuhumiwa wengine wanatafutwa ninpamoja na Halima Mdee, Zitto Kabwe na kuwataka wajisalimishe.