Tuesday, November 24, 2020

WHO yazungumzia chanjo dhidi ya Corona



Ghebreyesus amefanya mkutano na waandishi wa habari wa kila wiki kwa kutumia njia ya video kwenye makao makuu ya shirika huko Geneva, Uswizi.

Akielezea kufurahishwa kwake na habari chanya kutoka kwa tafiti za chanjo ya Covid-19, Ghebreyesus alionya kuwa kasi iliyoonyeshwa katika utengenezaji wa chanjo inapaswa pia kuonyeshwa katika usambazaji wao wa haki.

Ghebreyesus, akisisitiza kuwa hadi sasa katika historia haijatengenezwa chanjo ya haraka dhidi ya janga lolote, alisema,

"Kwa habari njema za hivi punde kutoka kwa majaribio ya chanjo, mwangaza mwishoni mwa handaki refu na la giza unazidi kung'aa. Sasa kuna matumaini ya kweli kwamba chanjo zitasaidia kumaliza janga hilo na hatua zingine zilizojaribiwa za afya ya umma."

Akisisitiza kuwa wanasayansi wamefikia kiwango kipya katika utengenezaji wa chanjo, Ghebreyesus, aliongeza kwa kusema,

"Jumuiya ya kimataifa sasa inapaswa kuweka kiwango kipya cha upatikanaji (wa chanjo)."


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...