Sunday, November 1, 2020

Sudan imesema imesaini na Marekani mpago wa kuzuia malipo ya fidia

 


Serikali ya Sudan imesema imetia saini makubalano na Marekani ambayo yatasimamisha kuendelea kulipa fidia zaidi, kutokana na kesi dhidi ya taifa hilo la Afrika zinazowasilishwa katika mahakama za Marekani, ikiwa ni baada ya serikali ya Marekani, kuliondoa taifa hilo katika orodha ya mataifa yenye kufadhili ugaidi. 

Waziri wa Sheria wa Sudan, Nasredeen Abdulbari amesema hatua hiyo inatekelezwa baada ya takribani mwaka mmoja wa majadiliano kati ya serikali ya Rais Donald Trump na uongozi mpya wa Sudan. Hatua hiyo itaanza kutekelezwa baada ya bunge la Marekani kupitisha sheria inayohitajika katika utekelezaji wa makubaliano hayo.

 Serikali ya mpito ya Sudan ilikubali kulipa dola milioni 335 kama fidia kwa waathirika wa mashambulizi ambayo yalifanywa na mtando wa al-Qaida, katika kipindi hicho kiongozi wa kundi hilo Osama bin Laden akiishi nchini Sudan.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...