Hadi jana Jumatatu, Biden alikuwa mbele ya Trump kwenye kura za maoni ya umma kuelekea uchaguzi wa leo unaofanyika chini ya kiwingu cha janga la virusi vya corona ambalo limewauwa mamia kwa maelfu ya watu nchini Marekani.
Trump, rais wa 45 wa Marekani anajivunia rikodi ya kuimarisha uchumi na kupunguza kwa kiwango kikubwa ukosefu wa ajira lakini anakosolewa kwa jinsi alivyoshughulikia janga la virusi vya corona.
Biden, mwanasiasa anayegemea sera za wastani za mrengo wa kushoto ameahidi kulinda haki ya wamarekani kupata huduma za afya, mafao kwa wazee na kutengeneza nafasi mpya za kazi kupitia sekta ya nishati .
Mchuano ni mkali na wasiwasi umetanda juu ya kuzuka mabishano baada ya uchaguzi huu, baada ya Rais Trump kutishia kujitangazia ushindi hata kabla ya matokeo kukamilika.
Credit: DW