Monday, November 2, 2020

Lebanon yaiunga mkono Uturuki dhidi ya Armenia

Wananchi wa Beirut wamekusanyika kupinga maandamano ya raia wa Armenia katika Ubalozi wa Uturuki nchini Lebanon, wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa habari, kikundi cha Waarmenia kilikusanyika mbele ya Ubalozi wa Uturuki mjini Beirut na kuanza kushambulia kwa mawe na fataki.

Hatua hiyo imeonekana kupingwa vikali na wananchi wa Lebanon,waliokusanyika kuiunga mkono Uturuki inayoiunga mkono Azerbaijan katika kukomboa maeneo yake yaliyokaliwa kimabavu na Armenia.

Wananchi wa Lebanon walikusanyika na kuimba wimbo wa taifa wa Uturuki na Lebanon, na kisha kuanza kutoa kauli mbiu za kumsifia raia wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan na kumuunga mkono harakati zake za kuisaidia Azerbaijan.

Mapigano yamekuwa yakiendelea kati ya Armenia na Azerbaijan, ambapo Armenia imekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano mara tatu.

Jeshi la Armenia limeripotiwa kuendeleza mashambulizi dhidi ya jeshi la Azerbaija na haswa katika maeneo ya raia wasiokuwa na hatia.

Takriban elfu 17 ya wanachi wa Mardin nchini Uturuki wanaoishi Beirut, walianza kuhamia Lebanon tangu miaka ya 1920, na sasa wana uraia wa Kituruki na Lebanon.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...