Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Madaba Bw. Mikael Hadu, na wataalam kutoka katika Halmashauri hiyo na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao Mapema leo Wilayani Madaba. |
Na Mwandishi wetu– MADABA
IMEELEZWA kuwepo kwa fursa nyingi za kilimo cha umwagiliaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma, kutokana na kuwepo kwa eneo kubwa lenye mabonde yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji licha ya maeneo hayo kutoendelezwa.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Bw.Mikaeli Hadu, alipokuwa akizungumza na wataalam kutoka Tumeya Taifa ya Umwagiliaji waliyopo katika ziara ya kikazi ya kutoa elimu na mafunzo katika baadhi ya skimu za wilaya hiyo wakianzia na skimu ya Hanga Nyadinda.
"Kuna fursa nyingi sana za kilimo hiki cha Umwagiliaji katika mkoa huu hasa kwa upande huu wa kuelekea Njombe, kwani mapori yanayofaa kwa kilimo ni mengi na wananchi wa maeneo haya ni wakulima wachapa kazi hivyo, Idara ya Umwagiliaji itakapokuwa katika zoezi la kuongeza eneo la Umwagiliaji ni vizuri ikaangalia maeneo haya katika jicho la kipekee na kuyaboresha, kwani wananchi wengi wamekuwa wakilima kienyeji, yaani kilimo cha vinyungu katika mabonde mengi hivyo eneo likiongezwa litahamasisha zaidi kilimo cha umwagiliaji." Alisema.
Bw. Hadu aliendelea kusema kuwa zipo skimu ambazo serikali imewekeza kwa ajili ya umwagiliaji lakin iwananchi hawa zitumii vizuri kitolea mfano wa skimu ya mbanga mawe, "Serikalii na tililia mkazo kilimo cha umwagiliaji ihivyo kuna kila sababu ya skimu hizi kufanya vizuri, wakulima wahamasishwe vya kutosha nakupewa elimuili uwekezaji huua mbao serikali imewekeza pesa nyingi ufanye kazi kwani utaboresha maisha ya wananchi." Alisisitiza.
Akiongelea swala la migogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Madaba, Bw. Hadu alisema mkoawa Ruvuma umekuwa na uingiaji mkubwa sana wa mifugo kutoka mkoa wa Mwanza, Simiyu na Rukwa na Halmashauri hii ndiyo lango kubwa sana la kupitisha Mifugo.
"Tumekuwa wakali sana kuhakikisha kuwa mifugo inayoingia ni yakuchinjwa na siyo ya kufuga lakini wafugaji ni wajanja wanachukua vibali kwa ajili ya kuleta ng'ombe wa kuchinja lakini wao wakiingia wanafuga, kwa hiyo tunaendelea saana kufuatilia jambo hili kwakushirikiana na Idara ya Mifugo ilikuweza kutatua migogoro inayojitokeza baina ya wakulimana wafugaji iliwote,wasipate madhara." Alibainisha.
Halmashauri ya wilaya ya Madaba ina skimu nne za kilimo cha umwagiliaji ambazo ni Luhimba, Ngadinda, Mbangamawe na Gumbiro zinazotajwa kuhitaji zaidi elimu kwa wakulima ambapo wataalam wakilimo cha umwagiliji walipata fursa ya kutoa elimu kuhusu Sheria ya Taifa ya Kilimo cha umwagiliaji na Mfuko wa maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji katika skimu ya Hanga Nyadinda..