Tuesday, November 24, 2020

Bunge la Uingereza laidhinisha vikwazo dhidi maafisa wa Nigeria

 


Maandamano ya kupinga ukatili wa polisi nchini Nigeria yalisababisha vuguvugu kubwa la kijamiiImage caption: Maandamano ya kupinga ukatili wa polisi nchini Nigeria yalisababisha vuguvugu kubwa la kijamii

Bunge la Uingereza limepiga kura ya kuunga mkono uwezekano wa serikali wa kuwawekea vkwazo maafisa wa Nigeria waliohusika katika madai ya matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa amani mwezi uliopita ya kupinga ukatili wa polisi.

Kura hiyo ilikuwa ni matokeo ya ombi lililoletwa mbele ya bunge la Uingereza ambalo lilisainiwa na watu zaidi ya 220,000.

Maafisa nchini Nigeria wameendelea kukanusha kwamba vikosi vya usalama viliwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa amani.

Wabunge wa Uingereza walisema kuwa vikwazo dhidi ya Nigeria vinaweza kuumiza umma wa Wanigeria.

Kwahiyo walitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru kuhusiana na unyanyasaji na wakaitaka serikali ya Uingereza kuwalenga maafisa waliohusika katika ufyatuaji wa risasi dhidi ya waandamanaji katika maandamano ya mwezi uliopita dhidi ya ukatili wa polisi.

Wabunge walirejelea mara kwa mara madai ya matumizi ya nguvu ya polisi dhidi ya waandamanaji katika eneo la Lekki tollgate mjini Lagos.

Pia walilaani kitendo cha kufuja akaunti za benki za waandalizi wa maandamano ya amani ambayo yalikuwa ni muhimu kwa demokrasia.

Baadhi ya wabunge walihoji nafasi ya Uingereza katika kutoa mafunzo kwa vikosi vya Nigeria na silaha kwa kwa nchi hiyo.

Mbunge aliyezungumza kwa niaba ya waziri wa Uingereza wa masuala ya Afrika aliafiki uamuzi wa Nigeria wa kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na kuvunjwa kwa kikosi tata cha polisi- cha kukabiliana na ujambazi.

Lakini bila utelezwaji wa wazo la kuweka vikwazo Wabunge walisema Uingereza itaendelea kushinikiza serikali ya Nigeria kuheshimu haki za binadamu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...