Na Faruku Ngonyani ,Mtwara.
Kuelekea siku ya uchaguzi Mkuu hapa unatarajia kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020 wasimamizi 195 wa vituo vya kupigia kura Jimbo la Mtwara wamekula kaipo cha utii na uadilifu.
Zoezi hilo limefanyika sambamba na kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo namna ya kujua na kutambua majukumu yao pindi watakapokuwepo kwenye vituo vya kupigia kura.
Kiapo cha utii na uadilifu kimeendeshwa na msimamizi wa jimbo la Mtwara Vijini Elica Yegella ambapo kwa furas hiyo amewasihii wasimizi hao wa vituo kuzingatia sharia na kanuni kwenye kazi yao ili kuepeka migongano kwenye vituo vyao.
Aidha kwa nafsi hiyo Yegella amewakumbusha wasimamizi hao wa vituo kuacha kuwa na upendeleo wa chama huku akiwasihii kutenda haki kwa wananchi wote watakaojitokeza siku hiyo juma tano ya kupiga kura.
Nae msimamizi msaidizi wa ambae pia mwezeshaji wa semina kwa wasimamizi hao wa vituo Ndg Hazzam Mambunga amwakumbusha wajibu wao siku yan kupiga kura ni pamoja na kuangali hali ya usalama wa kituo,kufunguliwa na kufunga kituo kwa muda ulipangwa na tume, kusimama sehemu ya kupigia kura na kuhakikisha shughuli zote ndani ya kituo zinaenda vizuri.
Lakini pia Hazzam amewakumbusha wasimamizi hao wa vituo kufunguliwa saa moja kamili asunhi na vitafungwa saa kumi kami ya jioni.