Monday, October 26, 2020
Wasimamizi Wa Vituo Vya Kupigia Kura, Makarani Waongozaji Wapewa Mafunzo
Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu Jimbo la Busega Anderson Njiginya Kabuko, amewataka wasimamizi, wasimamizi wasaidizi na makarani waongozaji wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu kuzingatia maelekezo na mafunzo yote wanayopewa ili kufanikisha zoezi la Uchaguzi mkuu wa tarehe 28/10/2020. Kabuko ameyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo tarehe 24/10/2020 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Bulima.
Aidha amewataka wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo kuwa makini na kutojihusisha na vitendo vitakavyowatia hatiana ikiwemo vitendo vya rushwa. "Katika kipindi hiki mnaweza kupata ushawishi mkubwa kutoka kwa makundi mbalimbali, ushawishi utakaoashiria vitendo vya rushwa, hivyo kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za usimamizi wa Uchaguzi", aliongeza Kabuko.
Wasimamizi, wasimamizi wasaidizi na makarani waongozaji wa vituo vya kupigia kura wamekula viapo mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Busega huku sehemu yao wakikiri kwamba mafunzo hayo yamewafanya kufahamu mambo mengi hivyo wanatarajia kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa.
Semina ya mafunzo kwa wasimamizi wakuu wa vituo na wasimamizi wasaidizi yanafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba 2020 katika ukumbi wa Shule ya Msingi Bulima na Silsos, lakini awali pia yalifanyika mafunzo ya Makarani waongozaji wa vituo vya kupigia kura ambapo mafunzo yalifanyika tarehe 24/10/2020 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Bulima.
Jumla ya wasimamizi wakuu, wasimamizi wasaidizi na makarani waongozaji wapatao 1,300 watashiriki katika Uchaguzi wa mkuu katika jumla ya vituo 325 jimbo la Busega.
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela amelishauri Kanisa la Kiinjili la Kilutheri ...
