Sunday, October 4, 2020

UWT Dodoma Mjini hakuna kulala, wachanja mbuga kusaka kura za CCM


 Kamati Maalum za vikao vya ndani vya Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Dodoma Mjini ikiongozwa na Katibu wake, Diana Madukwa imefanya ziara katika kata tatu z Msalato, Uhuru na Hazina na kuwafikia wanawake ambapo wamewaomba kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na madiwani wa chama hicho.

Akizungumza katika mikutano hiyo, Diana amesema kazi kubwa iliyofanywa na Magufuli kwa miaka mitano inatosha kabisa kujenga imani kwa watanzania ili aongezewe miaka mitano mingine ya kuwatumikia watanzania hasa wanyonge kama ambavyo amejitanabaisha.

Amesema Magufuli ni Rais ambaye hata nchi zingine zinatamani kuwa nae kwa jinsi alivyobeba maono makubwa ya kuwatumikia watanzania na zaidi jinsi alivyoivusha Nchi kwenye janga la ugonjwa wa Corona ambao mpaka sasa zipo baadhi ya Nchi zinateseka na kuwafungia watu ndani.

Huyu ni kiongozi ambaye Mungu amemleta kwetu kuja kutuvusha na amefanikiwa sana, kwenye Corona alisema tumtegemee Mungu na wala hakutufungia ndani kama Nchi zingine, akaruhusu shughuli zote za kijamii na kiuchumi kuendelea, Magufuli huyu huyu ametufikisha uchumi wa kati hata kabla ya muda wa malengo tuliojiwekea ambao ni 2025.

Tunapaswa kumpigia kura za kishindo na heshima, Dk Magufuli ili kumshukuru kwa yale makubwa aliyoyafanya ndani ya Jiji letu la Dodoma, leo tunaongoza kwa mtandao wa lami nchi nzima, tunajengewa kiwanja kikubwa cha ndege ambacho kitaongeza fursa za maendeleo kwenu wananchi, hakuna sekta ambayo Magufuli hajaigusa, twendeni tukampigie kura," Diana Madukwa.

Katibu huyo wa UWT pia amewaomba wananchi wa kata hizo kujitokeza kwa wingi kumchagua Mbunge Mavunde ambaye kwa miaka mitano amegusa maisha ya wananchi wa kada zote pamoja na kuleta maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo uchumi kwa kusaidia mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kuboresha sekta ya Afya na kukuza elimu ndani ya Jiji hilo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...