Saturday, October 3, 2020

Chama Tawala Nchini Kenya Chapendekeza Naibu Rais wa Kenya, William Ruto Aondolewe katika nafasi yake

Chama cha Jubilee kimependekeza Naibu Rais wa Kenya, William Ruto kuondolewa katika nafasi yake kama Naibu Kiongozi wa Chama hicho.

Katibu Mkuu wa Jubilee, Raphael Tuju amedai Ruto ni mjeuri, ana dharau na hamuheshimu Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta.

Chama hicho kimemshtumu Naibu huyo kwa kujaribu kufanya Mapinduzi wakati Rais Kenyatta akiwa katika safari ya kikazi nchini Ufaransa. Uongozi umesema Ruto hataruhusiwa kuingia katika Makao Makuu ya Chama.
 
Lakini wakiongea katika hafla moja mjini Nakuru, Magharibi mwa Kenya, ambayo pia ilihudhuriwa na makamu wa rais William, Ruto, Wabunge kadhaa na maseneta wanaomuunga mkono, wamepinga tangazo hilo la bwana Tuju, huku wakisema kuwa, katibu mkuu wa chama Tuju hana mamlaka hayo na kuwa ofizi za kitaifa za chama ni za wanachama wote.
 
Ruto ameanza kufanya kampeni zake za kuwania urais 2022. Lakini Rais Kenyatta amesisitiza kwamba sasa sio muda wa kufanya kampeni na badala yake kutimiza walichoahidi Wakenya. 


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...