Monday, June 1, 2020

Rais Trump kukutana na mwanasheria mkuu kuhusu hali nchini Marekani


R


Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia kukutana kwa faragha na msimamizi wake mkuu wa sheria leo, kufuatia maandamano ya vurugu yalioshuhudiwa katika miji kadhaa nchini humo, kupinga ubaguzi na ukatili wa polisi katika wakati huu wa janga la corona. 

Trump hajatoa tamko lolote kuzungumzi mzozo huo unaozidi lakini ameandika tweet kadhaa akiwaelezea waandamanaji kama vibaka na kuwahimiza mameya na magava kuchukuwa hatua kali zaidi. 

Alitishia pia kutumia jeshi lakini mshauri wake wa usalama wa taifa amesema serikali bado haiwezi kutumia udhibiti juu ya vikosi vya ulinzi wa taifa. 

Wakosoaji wamemlaumu Trump, ambaye anatafuta muhula wa pili kwa kuchochea mzozo na ubaguzi badala ya kuiunganisha nchi na kushughulikia masuala yaliopelekea hali hiyo. 

Machafuko yalioikumba nchi hiyo yamesababishwa na kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd, alieuwa na afisa polisi mweupe kwa kumkandamiza shingoni kwa goti lake kwa karibu dakika kumi, huku akirekodiwa na mpita njia. 

Sehemu tofauti za dunia pia zimefanya maandamano ya mshikamano na Wamarekani kupinga dhuluma dhidi ya jamii za wachache. 


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...