Wednesday, June 3, 2020

Mkoa wa Ruvuma una ziada ya chakula tani 900,000



Na Muhadh Mohammed. Songea Ruvuma.

MKOA wa Ruvuma hadi kufikia Mei mwaka huu una ziada ya chakula zaidi ya tani 900,000.
Hayo amesema na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme wakati anafungua kikao maaluma cha Baraza la  madiwani cha kujadili ripoti ya CAG Halmashauri ya Mbinga,kilichofanyika ukumbi wa Benjamini Mkapa katika shule ya sekondari Kigonsera .

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa hadi kufikia Mei 15 mwaka huu Mkoa ulikuwa umevuna zaidi ya tani milioni 1.4 za mazao ya chakula na biashara.

 ''Tunamshukuru Mungu ametupa Mvua nzuri na ametuepusha na wadudu wa haribifu hivyo tunatarajia kuvuna mazao mengi mwaka huu katika Mkoa wetu''.

 Hata hivyo Mndeme ametoa raia kwa  wakulima wajiepushe kuuza mahindi kwa bei ndogo kwa sababu mahitaji ya chakula  mwaka huu ni Makubwa na kwamba  walanguzi wananunua kwa bei ndogo hivyo wasifanye haraka kuuza.

Ametoa rai kwa wakulima kusubiri serikali itoe bei nzuri ili wananchi waweze kupata faida badala ya kunyonywa na walanguzi ambao  hivi sasa wapo wengi wanapita kwa wakulima ili kununua mazao kwa bei ndogo.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...