Friday, June 12, 2020
Merkel ataka fursa sawa ya kibiashara na China
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesisitiza usawa kwa Ujerumani na makampuni mengine yanayofanya shughuli za kibisahra nchini China katika mazungumzo yake kwa njia ya video na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang.
Msemaji wa kansela huyo, Steffen Seibert amsema katika mazungumzo hayo ya jana Merkel ametolewa wito Li kutoa fursa ya soko bora kwa makampuni ya kigeni nchini China, ambayo ni mshirika muhimu wa kibiashara wa Ujerumani. Kansela Merkel aliweka wazi kabisa, kwamba hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa katika kuboresha hali ya makampuni ya kigeni nchini humo na kusisitiza umuhimu wa kuwepo kwa makubaliano ya uwekezaji kati ya Ulaya na China.
Aidha kwa mujibu wa Seibert, Kansela Merkel alitilia mkazo pia matakwa ya Ujerumani katika kusimamia kanuni na biashara huria, kama ilivyosisitizwa katika maazimio ya Shirika la Biashara Duniani (WTO), na kuendeleza biashara madhubuti ya pamoja. Kwa mujibu wa chama cha wafanyabiashara cha Umoja wa Ulaya makampuni ya Ujerumani na Ulaya ambayo wasiwasi uliopo kwa sasa ni ongezeko la biashara zinazomilikiwa na serikali nchini China.
Mazungumzo baina ya viongozi hao wawili, ambayo yalihudhuriwa na Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Peter Altmaier, pia yaligusia janga la virusi vya corona na athari zake za kuuporomosha uchumi. Na hasa kujikitia katika mjadala wa kuchachua biashara baina ya mataifa hayo mawili, katika kipindi hiki cha mkwamo, na kugubikwa na uhusiano mbaya kati ya serikali za Marekani na China.
Mkutano mkubwa wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na China, ambao ulipaswa kufanyika mjini Leipzig nchini Ujerumani, Desemba ilisitishwa kutokana na mripuko wa janga la corona.Hata hivyo msemaji wa Merkel, Seibert amesema, miongoni mwa ajenda muhimu za Kansela Merkel katika mkutano huo na Li Keqiang ulizungumza suala la haki za binaadamu na hali ilivyo sasa mjini Hong Kong.
Kandoni mwa mkutano huo, wanasiasa kutoka katika katika kada mbalimbali walimtolewa wito Kansela Merkel kusimama kidete juu ya suala la uhuru wa Hong Kong, kwa muhtadha wa kitisho cha sheria ya usalama wa taifa ya China ambayo ilipigiwa kura mwezi Mei. Gyde Jensen, ambae ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya haki za binaadamu aliliambia shirika la habari la Ujerumani (DPA) wanamtarajia Merkel kulaani vikali mpango wa serikali ya China. Mwanasiasa huyo alisema serikali ya shirikisho la Ujerumani lazima itekeleze ahadi yake ya sera za mambo ya nje ya kuzilinda haki za binaadamu.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...