Wednesday, June 10, 2020

Azimio La Kumpongeza Rais Magufuli Kwa Mapambano Dhidi ya Corona Lapita Kwa Kishindo Bungeni

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Bunge limefanya   azimio La Kumpongeza  Rais   Wa  Jamhuri Ya  Muungano  Wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Kwa Namna Alivyoliongoza Taifa  Katika Mapambano Dhidi Ya Janga La UgonjwaWa Corona (Covid-19)


Akiwasilisha  azimio  hilo  jana  Juni 9,2020 Bungeni   jijini  Dodoma  mbunge wa VITI MAALUM  Esther  Mmasi  amesema  katika  kukabiliana  na  ugonjwa   wa Corona  Rais alitumia mbinu na mikakati mbalimbali ikiwemo  kukataa    kuiga  mtindo  wa kufunga mipaka  na  kuwafungia  wananchi  wake wasitoke nje tofauti na viongozi wa Mataifa mengine waliofunga  mipaka  ya nchi zao na  kuzuia watu wao kutokanje    (lockdown) .

Hivyo Mhe.Mmasi amesema kwa  kuzingatia hali hiyo, Rais Magufuli  aliruhusu  shughuli za kiuchumi  na  baadhi  ya  shughuli za kijamii    ziendelee  kwa  tahadhari  na  kuwahimiza wananchi kuzingatia  maelekezo na miongozo  ya wataalam.

Wakichangia Michango yao kuhusu mjadala wa  azimio hilo la kumpongeza Rais,baadhi ya Wabunge akiwemo Mbunge wa Rombo Mashariki Joseph Selasini amesema Rais Magufuli amesaidia kuondoa hofu kwa Watanzania ,mbunge wa Viti Maalum Christina Ishengoma akitoa pongezi kwa kuruhusu ibaada huku Mbunge wa Viti Maalum  Nagma Giga   akisema Rais Magufuli amekuwa Mzalendo wa Kweli kwa Taifa la Tanzania.
==>>Lisome Tamko Zima Hapo Chini


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...