Wednesday, June 10, 2020

Wabunge 69 wa CHADEMA Kuhojiwa Leo na Takururu.....


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Makao makuu Dodoma, leo inatarajia kuanza kuwahoji Wabunge na waliokuwa Wabunge  wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo kwa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TAKUKURU inasema wabunge hao watahojiwa kutokana na tuhuma mbalimbali ambazo zimetolewa na baadhi ya wabunge ambao wamehama chama hicho na kudai kuna fedha walikuwa wakichangishwa lakini matumizi yake hayajulikani.

"Tunapenda kuthibitishia umma kwamba ni kweli kuwa TAKUKURU Makao makuu imewaita waheshimiwa wabunge wa CHADEMA na waliowahi kuwa wabunge wa chama hicho kwa mahojiano" imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inasema mahojiano hayo ni mwendelezo wa uchunguzi unaoendeshwa na TAKUKURU Makao makuu wa malalamiko dhidi ya matumizi ya fedha za chama na hatua ya Sasa ni kuhoji wabunge sitini na tisa(69).

Kwa mujibu wa malalamiko hayo wabunge hao wanadai walikuwa wakikatwa kwa wabunge viti maalumu walikuwa wakikatwa kiasi Cha milioni moja laki tano na sitini(1,560,000) na wabunge wa kuchaguliwa walikuwa wakikatwa laki tano na ishirini (520,000).

Na wabunge hao walidai kutojua matumizi ya fedha hizo, na kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa TAKUKURU Brigedia Jenarali John Mbungo, Mei 27, 2020 kwamba uchunguzi tayari ulishaanza na baadhi ya viongozi wameshahojiwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU yataanza kufanyika leo TAKUKURU Makao Mkuu Dodoma na yanatarajiwa kukamilika wiki ijayo
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...