Monday, May 4, 2020

WATOA HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA WAPEWA MAFUNZO NAMNA YA KUHUDUMIA WASHUKIWA NA WAGONJWA WA CORONA

Jumla ya watoa huduma za afya 56 kutoka kwenye vituo vya afya vya umma na watu binafsi wilaya ya Shinyanga na Kishapu wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutoa matibabu kwa washukiwa na wagonjwa watakaobainika kuwa na Maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID 19).

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa ufadhili wa Shirika la Lifewater International yamefanyika leo Jumatatu Mei 4,2020 katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Afisa Afya Mkoa wa Shinyanga Neema Simba amesema mafunzo hayo yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma za afya wawe tayari kuhudumia washukiwa wa ugonjwa wa Corona.

"Tunawashukuru Lifewater International kwa ufadhili wa mafunzo haya ambayo yamekutanisha watoa huduma za afya kutoka kwenye vituo vya afya vya umma na binafsi katika Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga",ameongeza Bi. Neema.

Naye Meneja wa Shirika la Lifewater International mkoa wa Shinyanga, Benety Malima amesema watoa huduma za afya ni kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee kwani wapo hatarini kupata maambukizi ya COVID 19 hivyo ni vyema wakajengewa uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa wa Corona.

"Lifewater International tumeamua kufadhili mafunzo haya kwani tunaamini sekta ya afya ni sekta ambayo ipo mstari wa mbele zaidi katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona. Watoa huduma za afya ndiyo wapo mstari wa mbele katika kuhudumia washukiwa na wagonjwa wa Covid 19",amesema Malima.

Kwa upande wake, Mratibu wa Huduma za Matibabu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee amesema miongoni mwa mada zitakazofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na Utambuzi wa washukiwa na wagonjwa wa Corona na namna ya kuchukua tahadhari kwenye maeneo yao ya kazi ili wasipate maambukizi.

Amesema pia watoa huduma wa afya watafundishwa namna ya kufanya matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga na maambukizi (Personal Protective Equipment - PPE) pamoja na namna ya kuvaa nguo/vazi maalumu linalotumika kuhudumia mshukiwa/mgonjwa wa Corona.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Afya Mkoa wa Shinyanga Neema Simba akizungumza leo Jumatatu Mei 4,2020 wakati  wa mafunzo kwa watoa huduma za afya kutoka kwenye vituo vya afya vya umma na watu binafsi wilaya ya Shinyanga na Kishapu yenye lengo la kuwajengea uwezo watoa huduma za afya namna ya kutoa matibabu kwa washukiwa na wagonjwa watakaobainika kuwa na Maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID 19). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Huduma za Matibabu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee akizungumza wakati wa mafunzo  kwa watoa huduma za afya wilaya ya Shinyanga na Kishapu ambapo amesema miongoni mwa mada zitakazofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na Utambuzi wa washukiwa na wagonjwa wa Corona,namna ya kuchukua tahadhari kwenye maeneo yao ya kazi ili wasipate maambukizi,matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga na maambukizi (PPE) pamoja na namna ya kuvaa nguo/vazi maalumu linalotumika kuhudumia mshukiwa/mgonjwa wa Corona.
Meneja wa Shirika la Lifewater International mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akizungumza wakati wa mafunzo kwa watoa huduma za afya ambapo amesema watoa huduma za afya ni kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee kwani wapo hatarini kupata maambukizi ya COVID 19 hivyo ni vyema wakajengewa uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa wa Corona.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Katibu wa Afya Mkoa wa Shinyanga William Mambo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Katibu wa Afya Mkoa wa Shinyanga William Mambo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Dkt. Geofrey Mboye akitoa mada kuhusu COVID 19.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Dkt. Geofrey Mboye akitoa mada kuhusu COVID 19.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Afisa Afya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Musa Makungu akitoa mada kuhusu COVID 19
Mafunzo yanaendelea.
Mafunzo yanaendelea.
Mafunzo yanaendelea.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
 Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...