Wednesday, May 6, 2020

Wakimbizi nusu milioni Kenya hatarini kuambukizwa COVID-19



Karibu wakimbizi nusu milioni wanaoishi katika kambi za wakimbizi Kenya wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19.

Kwa mujibu wa taarifa wakimbizi hao wanaaishi katika kambi zenye msongamano mkubwa wa watu na suhula duni za kiafya ya kijamii.

Hadi sasa hakuna kesi ya corona iliyoripotiwa katika kambi hizo lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)  limetangaza kuna mipango ya kukabiliana na COVID-19.

UNHCR imetahadharisa kuwa, maafa makubwa yataibuka iwapo ugongwa wa COVID-19 utaenea miongoni mwa wakimbizi.

Kambi ya Dadaab iliyoko kaskazini mashariki mwa Kenya ina wakimbizi  211,365 waliosajiliwa na hivyo kuifanya kuwa kambi ya tatu kwa ukubwa duniani. Kambi nyingine kubwa ya wakimbizi nchini Kenya ni ile ya Kakuma iliyo kaskazini mwa nchi hiyo na inakadiriwa kuwa na wakimbizi 194,000. Aghalabu ya wakimbizi nchini Kenya ni kutoka nchi jirani za Somalia na Sudan Kusini.

Hadi sasa watu 535 wameambukizwa COVID-19 na miongoni mwao 182 wamepona na  wengine 24 wameaga dunia.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...