Wednesday, May 27, 2020

Ufaransa yapiga marufuku dawa ya hydroxychloroquine



Serikali ya Ufaransa leo imefuta amri inayowaruhusu madaktari katika mahospitali kutumia dawa ya Hydroxychloroquine kama tiba kwa wagonjwa walioko katika hali mbaya ya kuugua ugonjwa wa COVID-19, ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona. 

Hatua hiyo, ambayo inaanza mara moja , ni ya kwanza kuchukuliwa na nchi, tangu shirika la afya ulimwenguni WHO kusema siku ya Jumatatu linasitisha kwa muda majaribio makubwa ya dawa hiyo ya malaria kutibu wagonjwa wa COVID-19 kutokana na wasi wasi juu ya usalama wake. 

Kufutwa kwa amri hiyo, ambayo kimsingi ina maana dawa hiyo sasa imepigwa marufuku kutumiwa, kulitangazwa katika taarifa rasmi ya serikali na kuthibitishwa katika taarifa na wizara ya afya. 

 Ufaransa iliamua mwishoni mwa mwezi Machi kuruhusu matumizi ya Hydroxychloroquine, ambayo pamoja na malaria pia imeidhinishwa kutibu magonjwa mengine maalum na katika hospitali inatibu wagonjwa wa COVID-19. 


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...