Wednesday, May 27, 2020
Maskini Juma Pondamali KOCHA wa Makipa Aishtaki Young Africans
Aliyekua kocha wa makipa Young Africans Juma Pondamali amelazimika kuishtaki klabu hiyo kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), kushinikiza kulipwa mshahara wake wa miezi saba.
Pondamali ambaye ni mlinda mlango wa zamani wa klabu hiyo kongwe nchini, alitimuliwa mwaka jana baada ya klabu hiyo kuvunja benchi lote la ufundi lililokuwa chini ya kocha Mwinyi Zahera.
Kocha huyo anayeinoa African Sports kwa sasa, amesema kuwa baada ya kuona hakuna dalili za kulipwa madeni yake, ameamua kupeleka suala hilo TFF anakoamini atapata haki yake.
"Wakati tunaondolewa nilikuwa nikidai mshahara wa miezi saba, uongozi ulisema utanilipa ndani ya muda mfupi lakini imekuwa tofauti na makubaliano," amesema Pondamali.
Amesema kabla ya uchaguzi mkuu wa mwisho kufanyika kwenye klabu ya Young Africans walifanya kazi katika mazingira magumu ikiwamo kutolipwa mshahara kwa miezi hiyo saba.
"Klabu ilikuwa kwenye hali ngumu na tulifanya kazi kwa mazingira hayo hayo, tukiamini uongozi mpya ukiingia madarakani utatulipa, lakini ikawa tofauti, tukaishia kuondolewa.
"Tuliambiwa baada ya siku chache tutalipwa fedha zetu, lakini imekuwa ndivyo sivyo na binafsi nimeona sina njia nyingine ya kupata haki yangu zaidi ya kwenda kushtaki TFF," anasema.
Mwenyekiti wa Young Africans, Dk Mshindo Msolla alikiri klabu hiyo kudaiwa.
"Si Pondamali pekee ambaye anatudai, klabu inadaiwa na watu mbalimbali na madeni yote tunayatambua na tutayalipa," anasema Dk Msolla.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...