Tuesday, April 21, 2020
Ukweli Mbosso Kupewa Gari la Tanasha na Diamond...
MAMBO ni mengi sana mjini. Unaambiwa wananzengo wamepiga kelele sana huko Instagram kwamba gari analotamba nalo staa wa Bongo Fleva, Yusuph Mbwana 'Mbosso' si mali yake, bali amepewa na bosi wake Nasibu Abdul 'Diamond' na ni lile alilokuwa amezawadiwa aliyekuwa mpenzi wa Mondi, Tanasha Donna! Risasi limechimba mambo.
Awali, Diamond gari hilo jipya aina ya Toyota Land Cruiser Prado, lilianza 'kutrendi' mitandaoni kwa maelezo ya kwamba, ni la Mbosso ndipo wananzengo walipoanza kukinukisha.
Watu walichukua picha ya gari hilo na kuanza kujiongeza na habari zao mbalimbali kwa kusema hana uwezo wa kununua gari hilo.
Kuna ambao walisema gari hilo ni la mama Diamond, hivyo mondi amewarusha tu roho mashabiki.
Wengine wakasema gari hilo amepewa na Diamond, kwani ni lile alilokuwa amezawadiwa Tanasha wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa, Julai 7, mwaka jana.
"Hili ni lile la Tanasha na kama unakumbuka, Tanasha alisema hana mpango nalo kwani anayo magari mengine kule kwao Kenya sasa naona mzee baba (Diamond) ndio kaamua kumpa Mbosso," alichangia mdau mmoja mtandaoni na kuungwa mkono na wenzake wengi.
Siku hiyo, mbali na Diamond kumzawadia Tanasha gari hilo, pia alimzawadia mama yake Sanura Kassim 'Sandra' gari kama hilohilo kwani naye alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Magari hayo, yote yalikuwa ni aina moja Toyota Land Cruiser Prado na yote yalikuwa meupe huku yakiwa yamewekwa plate namba za majina yao.
Hata hivyo, wakati zogo likiwa kubwa mtandaoni, Diamond aliposti gari hilo kwenye Insta Story yake na kueleza kwamba ni mali ya Mbosso, hivyo kuwakata vilimilimi waliokuwa wanasambaza habari hizo za uongo.
Baada ya maneno kuwa mengi mitandaoni, Risasi Jumamosi lilimvutia waya Mbosso ambaye alifunguka ukweli wake.
Risasi Jumamosi: Juzikati kuna gari la thamani ambalo Diamond aliliposti kwenye ukurasa wake wa Instagram na akasema ni la kwako, lakini wananzengo walianza kutia maneno ya kejeli, wewe una lipi la kuzungumza kuhusiana na suala hilo?
Mbosso: Ni kawaida tu kwenye maisha mtu kutoamini kile ambacho wanakiona, ila nadhani sasa hivi wameamini kile ambacho Diamond amekionyesha kwa sababu watu walikuwa wanasema kwamba lile gari ni la Tanasha na wengine wanasema ni la mama Diamond. Lile gari ni langu na watu waache kuongea maneno wasiyoyajua, yale magari ni aina tatu tofauti kabisa, nina imani zile kelele za kujadili gari langu zitaisha.
Mbosso alisema magari hayo yanafanana kwa aina lakini kila mtu ana lake, hivyo watu waache kuongea vitu ambavyo hawana uhakika navyo.
Mbosso hakutaka kueleza thamani ya gari hilo lakini akasisitiza tu ni lake na yeye ndio anayelimiliki.
STORI: IMELDA MTEMA, RISASI
Source
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 29, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...