Tuesday, April 21, 2020

DC Daqqaro awaka ujenzi wa zahanati kusimama zaidi ya miaka 12

Na Alphonce Kusaga

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro  amehoji ni kwanini zahanati ya Baraa ujenzi wake ulisimama zaidi ya miaka 12 ilhali hadi sasa halmashauri ya Jiji la Arusha imetoa zaidi ya sh, milioni 84.120

Daqqaro amesema hayo katika Kata ya Baraa wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya elimu, Afya na Miradi ya Kimkakati (TSCP) iliyoambatana na wataalam wa Jiji la Arusha.

Daqaro amehoji katika kipindi cha miaka 12 wananchi wa kata ya Baraa wanakosa huduma za Afya na kulazimika kupata huduma hizo kata ngingine.

"Nataka kujua ni kwanini ujenzi umechukua muda mrefu huku wananchi wakishindwa kupata huduma za afya katika eneo la karibu na makazi yao"

Kwa upande wa Injinia Samuel Mshuza amesema awali kulikuwa na vipaumbele vingine vilivyopelekea zahanati hiyo kutokamilika kwa wakati pia ramani ya jengo hilo ilibadilishwa lakini sasa wapo katika hatua za mwisho za ujenzi wa zahanati hiyo

Naye Mtendaji wa Kata hiyo ya Baraa, Anna Lebisa alisema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo ulianza kutekelezwa  mwaka 2008na kusimama kwa zaidi ya miaka 12 lakini hivi sasa wanaishukuru serikali kwa kutekeleza ujenzi huo kwa zaidi ya asilimia 86 ambapo amesema eneo hilo kunachangamoto ya udongo sambamba na maji kutuama

Hata hivyo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk, Maulid Madeni alisema kuwa fedha za ujenzi wa zahanati hiyo zipo na kuwataka wakandarasi wa zahanati hiyo ya Baraa na Hospitali ya Wilaya ya Arusha kusema wanahitaji kiasi gani cha fedha ili waweze kulipwa na ujenzi uendelee

"Namshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa hospitali na vituo vya afya Mkoa wa Arusha ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru iliyopo Jijini Arusha" Alisema DC Daqaro

Pia Amesisitiza jengo la wadi ya kinamama na mtoto katika hospitali ya wilaya kumalizika mapema ili kuondoa msongamano katika hospitali ngingine
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...