Tuesday, April 21, 2020

Wabunge wa Uingereza kushiriki vikao kwa njia ya video

Wabunge wa Uingereza wapiga kura kuchelesha Brexit | Muhabarishaji

Bunge la Uingereza linarejea leo baada ya mapumziko ya Pasaka huku wabunge wakihimizwa kutumia njia ya video kushiriki shughuli zilizopangwa ikiwa ni matokeo ya mlipuko wa virusi vya corona.

 Kanuni za jamii kujitenga zinataka kuwepo umbali wa mita mbili baina ya watu sharti ambalo linalomaanisha ukumbi wa bunge mjini London hautokuwa na nafasi ya kutosha kwa idadi ya wabunge 650.

 Wabunge wa nchi hiyo wametakiwa kutumia njia ya video kushiriki mijadala hatua ya kwanza kuchukuliwa katika historia ya miaka 700 ya uwepo bunge la Uingereza.

Uingereza bado imeweka marufuku dhidi ya shughuli za kawaida kufutia mlipuko wa virusi vya corona ambavyo vimewauwa zaidi ya watu 16,500 na wengine wengi kuambukizwa ikiwemo waziri mkuu Boris Johnson.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...