Friday, July 5, 2019

Jengo jipya la tatu JNIA kuanza kutumika mwezi ujao


Naibu Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi  Atashasta Nditiye, amesema Ujenzi wa Jengo la  tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha  Julius Nyerere (JNIA) umekamilika,  na Jengo linatarajiwa kuanza uendashaji mwanzoni mwa mwezi Agosti  mwaka huu.

Pia amesema amefurahishwa  kwa  kukamilika kwa jengo hilo  ambapo  ni la  kisasa na huduma zake zake ni nzuri.

Akizungumza mara  baada ya Ziara ya kukagua Jengo hilo , amesema katika idadi ya miruko ya ndege Barani Afrika  JNIA inachukua nafasi ya tano  na nafasi ya sita kwa idadi ya abiria.

''Nimefurahishwa kwa kukamilika kwa Ujenzi wa jengo la tatu la abiria wa  Kiwanja cha Ndege ambapo utakapoanza kuhudumia abiria natarajia tutachukua nafasi nzuri zaidi Barani Afrika kwani ni Jengo la kisasa na litatoa huduma nzuri,'' alisema.

Nae Mkurugenzi  wa Kiwanja cha Ndege cha  Kimataifa cha Julius Nyerere ( JNIA), Paul  Rwegasha akitoa ufafanuzi wa Kiwanja hicho, alisema  mara baada ya kukamilika kwa jengo la tatu itakuwa jumla ya majengo matatu  yanaweza kuhudumia abiria milioni nane kwa mwaka.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama, alisema kwasasa kuna  katika maandalizi ya Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa 39 wa SADC  ambapo maadalizi yameambatana na ukarabati wa maboresho ya miundombinu  na samani.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...