Jeshi la polisi mkoani Pwani ,linamtafuta mwanamke ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua mtoto wake Halima Ramadhani (5) kwa tuhuma za kuunguza pazia la chumbani.
Kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha huko Kikongo wilaya ya Kipolisi Mlandizi wilayani Kibaha
Alisema mama huyo , alimuua mwanaye kwa kipigo akimtuhumu mwanaye huyo kuunguza pazia hilo kwa kutumia kibatari.
"Baada ya kukuta pazia hilo limeungua mama yake alimshambulia na kupelekea kifo cha mtoto huyo na alipoona hali mbaya alikimbia," alisema Nyigesa.
Alisema,mtoto huyo alifariki alipofikishwa katika kituo cha Afya Mlandizi siku hiyo hiyo majira ya saa nne usiku.
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani