Thursday, October 25, 2018
Shirika la bima la taifa latoa ushauri wa bure kwa wamiliki wa viwanja vya michezo
Na.Ahmad Mmow, Lindi
SHIRIKA la bima la taifa (NIC) licha ya kuchangia shilingi 10,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa halmashauri ya wilaya Ruangwa mkoa wa Lindi limetoa wito kwa wamiliki wa viwanja vya michezo nchini kuvikatia bima viwanja hivyo.
Wito huo umetolewa leo mjini Ruangwa na meneja wa bima wa tawi la Lindi, Azaria Mpolenkile aliyemuwakilisha mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo (Sam Kamanga) wakati wa hafla ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi 10 milioni kwa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kwaajili ya ujenzi wa uwanja huo wa mpira hafla ambayo ilifanyika mjini Ruangwa.
Mpolenkile alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wamiliki wa viwanja vya michezo nchini kukatia bima viwanja wanavyomiliki ili kuwahakikishia fidia watazamaji wanaokuwa ndani ya viwanja hivyo wakati wanaangalia michezo, ili wawe na uhakika wakufidiwa pindi ikitokea ajali.
Alisema ndani ya viwanja vya michezo kunakuwa na watu wengi wanaoingia kwenda kuangalia michezo Hata hivyo kunaweza kutokea ajali ambazo zinaweza kusababisha watu hao kujeruhiwa na kuwasabishia ulemavu na wengine kufa.
Source
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...