Wednesday, October 10, 2018

KUWA NA WAPENZI WENGI NI UGONJWA WA AKILI


Kitendo cha kumsaliti mpenzi wako au Kutamani kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja kumetajwa ni miongoni mwa matatizo yanayoweza kusababishwa na magonjwa ya akili endapo mshiriki wa vitendo hivyo atashinikizwa na matamanio ya kimwili yatakayotokana na hali ya mazingira.

Hii ni kwa mujibu wa mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Debora Lwambano ambaye amesema kuwa hali hiyo hutokea pale mtu anapoendeshwa na hisia bila yeye mwenyewe kujijua.

"Kuna vitu vingine ni tabia ila ukiona mtu anatamani kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja au kushirikii mapenzi zaidi ya mtu mmoja nayo tunaweza kusema ni ugonjwa wa akili kama yatasababishwa na mahitaji ya kimwili yanayotokana na mtu kuwa mtumiaji sugu jambo fulani", amesema Debora.

"Katika matatizo ya akili ya sonona na mania, kama mtu anafanya mapenzi zaidi ya mtu mmoja, ina dalili zake na inaweza isipatikane moja moja, unakuta mtu anakuwa na hamu sana ya kufanya mapenzi zaidi ya mpenzi mmoja ila lazima tuangalie na dalili zingine." amesema.

Mbali na kushiriki mapenzi zaidi ya mpenzi mmoja pia tabia ya watu wengi kushiriki punyeto (masturbation) pia ni matatizo yanayosababishwa na ugonjwa wa akili.

"Kwa haraka haraka tunaweza kusema punyeto pia inatokana na matatizo ya ugonjwa wa akili, yanayosababishwa na mtu kuangalia picha na video za ngono mara kwa mara, na kumfanya mtu kuwa mlevi wa kushiriki kitendo hicho kunakoweza kumpelekea kushindwa kushiriki kwa muda mrefu kwenye tendo lenyewe", ameongeza Debora.

Chanzo - EATV

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...