Wednesday, August 22, 2018

Muziki wa Bongo Fleva Umepungua Kasi.:-Ali Kiba

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini, Alikiba anasema kuwa anaona kuwa kasi ya muziki wa bongo fleva imepungua kasi hasa kutokana na kukosekana kwa tuzo zilizokuwepo zilizokuwa zikihamasihsa wasanii kufanya muziki kwa umakini zaidi. Alikiba anayetamba na kibao chake cha Mvumo wa Radi ameyasema hayo katika mahojiano na Azam Tv mwezi huu wa Agosti kupitia kipindi cha Nyundo ya Baruan. "Mwendo wa muziki wa Bongo Flava unakwenda vizuri ijapokuwa kuna watu wanachanganya tu muziki na wengine wanaaribu muziki na wengine wanakwenda nao vizuri lakini hiyo pia siwezi kuichambua kwa sababu kila mtu anakipaji chake," amesema Alikiba Alikiba ameongeza "Wengine wanafanya kwa kujifurahisha na wengine wanafanya kwaajili ya maisha yao lakini muziki kidogo umepungua nguvu." "Ninaimani kwa sababu ya tuzo za Tanzania zilikuwa zinawahamasisha sana watu, wasanii walikuwa wakifanya kazi vizuri na kwa bidii anaamini kwamba siku moja ataitwa na atapewa heshima unajua tuzo ni heshima tu." "Kwa hivyo changamoto kidogo imepungua, kasi imepungua ni kutokana na tuzo kwa vijana maana mtu anaweza kujitungia nyimbo yoyote ambayo haina kichwa wala miguu sababu hategemei chochote lakini pia kampuni yangu ya Mo Faya inamipango hiyo ya kuwahamasisha vijana kufanya tuzo baadae Insha allah." Mwanamuziki huyo anayefanya vizuri barani Afrika amesema kuwa wasanii anao wakubali kutoka katika bara hili ni Oliver Mtukudzi kutoka Zimbabwe na mama Yvonne Chaka Chaka wa Afrika Kusini.      

The post Muziki wa Bongo Fleva Umepungua Kasi.:-Ali Kiba appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...