Taarifa zilizopatikana muda huu zinasema Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangwallah amepata ajali asubuhi hii akitokea Arusha katika eneo la msitu kabla ya kijiji cha Magugu maarufu kama Mguu wa Mjerumani ama Mdori.
Kwa mujibu wa mbunge wa Mbulu vijijini Mhe. Flatei Massay mtu moja ambaye ni mwandishi wa habari amepoteza maisha.
Inasemekana chanzo cha ajali hiyo ni Twiga aliyekuwa anakatisha barabara mbele yao na katika kumkwepa gari likapinduka.
Taarifa zinapasha kuwa Dkt. Kigwangwala amepata majeraha ya mkono na kifua na kukimbizwa katika kituo cha afya cha Magugu kupatiwa matibabu na kwa mujibu wa mleta habari, hali sio nzuri sana.
Hivi sasa inasubiriwa helikopta ije kumchukua kumpeleka hospitali kubwa.
Source