Saturday, August 4, 2018

UPDATES YA AJALI: WAZIRI KIGWANGALA APATA AJALI, MWANDISHI WAKE AFARIKI DUNIA

* Dk. Kigwangala aumia shingoni, mbavuni, mkononi
*Chanzo cha ajali dereva wake kukwepa Twiga barabarani

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

PIGO kubwa Wizara ya Malialisi na Utalii! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya kutoke ajali ya gari aliyokuwa akisafiria Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala ambayo imesababisha kifo cha Ofisa Habari wa Wizara hiyo.
Katika ajali hiyo ya gari kulikuwa na watu sita akiwamo Waziri Kigwangala ambaye ameumia katika mbavu, mkono na shingo na kwa sasa anapatiwa matibabu wilayani Manyara wakati wanaandaa utaratibu wa kumhamishia yeye pamoja na majeruhi wengine katika hospitali kubwa kwa matibabu zaidi.
Akizungumza kwa njia ya simu asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Augustino Senga amesema Waziri Dk.Kigwangala alikuwa anatokea mkoani Arusha kuelekea mkoani Dodoma na alipofika eneo hilo gari yao ikatapa ajali hiyo.
Amefafanua kwa sasa ndio yupo njiani anaelekea eneo ambalo ajali imetokea lakini kwa mujibu wa wasaidizi wake ni kwamba ajal hiyo imesababisha kifo cha mwandishi wa Waziri Kigwangala.
Hata hivyo hajataja jina lake.Wakati tukisubiri jina kamili ya aliyefariki kwenye ajali hiyo kutoka kwa Kamanda Senga taarifa zilizipo mitandaoni zinaeleza aliyefariki ni Ofisa Habari wa Wizara hiyo (Mwandishi Hamza Temba.
Alipoulizwa chanzo cha ajali hiyo Kamanda Senga amesema taarifa alizonazo ni kwamba eneo hilo kuna hifadhi ya wanyama na hivyo wakati gari ya Waziri inapita kulikuwa na mnyama barabarani na hivyo dereva akawa anajaribu kumkwepa.
"Wakati anamkwepa ndipo gari ilipomshinda dereva na kusababisha kupoteza muelekeo na hivyo kupinduka na kusababisha kifo cha mwandishi huyo na wengine kujeruhiwa akiwamo Waziri Kigwangala ambaye anapatiwa matibabu pamoja na dereva wake.
"Nikifika eneo la tukio nitakuwa na nafasi nzuri ya kutaja majina ya waliokuwamo kwenye gari hilo na hali zao kiafya. Lakini hadi sasa tunazo taarifa za kifo cha mtu mmoja ambaye ni mwandishi wa Waziri,"amesema Kamanda Senga.
Pichani juu na chini ni Gari la Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangwallah ambaye amepata ajali asubuhi hii akitokea Arusha katika eneo la msitu kabla ya kijiji cha Magugu maarufu kama Mguu wa Mjerumani ama Mdori. Kwa mujibu wa mbunge wa Mbulu vijijini Mhe. Flatei Massay alieleza kuwa mtu moja ambaye ni mwandishi wa habari amepoteza maisha. Inasemekana chanzo cha ajali hiyo ni Twiga aliyekuwa anakatisha barabara mbele yao na katika kumkwepa gari likapinduka.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...