Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, amewaonya watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA wanaojihusisha na vitendo vya ukosefu wa maadili vinavyochangia kuikosesha serikali mapato yake yatokanayo na kodi, vikiwemo vitendo vya rushwa na kwamba watachukuliwa hatua.
Bw. James, ametoa kauli hiyo wakati akihitimisha kikao maalum kati ya Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango, Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Menejimenti pamoja na Mameneja wa Mikoa yote ya Tanzania Bara wa Mamlaka hiyo.
Amesema kuwa vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo ikiwemo vitisho kwa wafanyabiashara wakati wa kukusanya kodi havikubaliki na kwamba Serikali ya ya awamu hii imejipanga kukabiliana navyo kwa nguvu zote hivyo watakaobainika wataambulia hatua kali za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi..
Aidha imeelezwa kwamba mpaka sasa tayari wafanyakazi kadhaa wa Mamlaka hiyo wamefukuzwa kazi huku wengine wakihamishwa vituo vyao vya kazi kutokana na mwenendo wao usioridhisha na kulalamikiwa kutofuata maadili yao ya kazi wakati wanatekeleza majukumu yao.
Mbali na hayo, Katibu Mkuu huyo ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kuhakikisha kuwa inafikia malengo ya kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 18 katika mwaka huu wa Fedha wa 2018/2019, ikiwa ni sehemu ya Bajeti ya shilingi trilioni 32.47, iliyopitishwa na Bunge ili kutekeleza majukumu mbalimbali ya Serikali ikiwemo miradi ya maendeleo.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...