Monday, March 3, 2025

Vuta Picha Sowah Kujiunga Yanga, Nani Atampisha?



Ebu vuta picha msimu ujao katika safu ya ushambuliaji ya Yanga yenye Prince Dube na Clement Mzize wenye jumla ya mabao 20 akiongezeka Jonathan Sowah ambaye ameanza kuonyesha makali yake Ligi Kuu akiwa na Singida Black Stars.
.
Sowah amekuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na viongozi wa Yanga tangu msimu uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakati huo mshambuliaji huyo alikuwa akiichezea Medeama ya Ghana anakotoka, lakini dili hilo lilikwama akatua Libya alikojiunga na AlNasr.
.
Tofauti kabisa na Mzize na Dube ambao wanaweza kutokea pembeni na kunyumbulika, Sowah ni mshambuliaji wa kati asilia mwenye sifa maalumu za kupambana na mabeki wagumu. Ana uwezo mkubwa wa kutumia mwili wake, hasa katika kumiliki mipira ya angani na kuvunja minyororo ya mabeki kwa mabavu. Hii inamfanya kuwa mchezaji hatari katika maeneo ya mbele ya lango, kwani anaweza kupambana na mabeki katili.
.
Nani atampisha? Taarifa za ndani zinasema, Sowah anayemiliki mabao manne kwa sasa tangu aanze kuitumikia Singida Black Stars, atachukua nafasi ya Kennedy Musonda.

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...