Tuesday, March 4, 2025

Alex Ngereza; Aucho Hawezi Mzuia Mpanzu, Ataambulia Kadi Nyekundu



Mchambuzi wa TV3 Alex Ngereza amemchambua mchezaji wa Yanga Sc Khalid Aucho,Alex Ngereza amesema.

"Sidhani kama Khalid Aucho anaweza kumaliza dakika 90 bila kadi nyekundu kwenye mchezo wa derby na kitu ambacho kinaweza kusababisha apate kadi ni ile speed ya viungo washambuliaji wa Simba"

"Khalid Aucho sio kiungo mwenye speed sana ndio maana mara nyingi anacheza sana rafu akikutana na viungo ambao wanakimbia sana au wenye control nzuri ya mpira"

"Ukiwatazama Simba, utagundua kwamba ni timu ambayo ina shambulia kwa idadi kubwa wachezaji na wote ni wachezaji wenye kasi kubwa kwanzia eneo la katikati na pembeni ya uwanja"

"Kama Elia Mpanzu atakuwa anaingia ndani sana kwenye ile halfu space kama ambavyo anacheza kwenye michezo mingine tafsri yake ni kwamba ataenda kukutana moja kwa moja na Khalid Aucho na kwa ubora wake Khalid Aucho hawezi kumzuia Mpanzu bila kumpiga boot"
-
"Mbaya zaidi mawinga wote wa Simba wana tabia ya kuingia sana ndani kitu ambacho sioni kama kinaweza kumuweka Khalid Aucho sehemu salama na ukiachan na hawa ambao wanatokea pembani yupo Jean Charles ambaye ni mchezaji hatari sana akiwa na mpira mguuni kwake"

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...