Wednesday, August 4, 2021

Zuma kuruhusiwa kutoka gerezani kuhudhuria kesi

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ataruhusiwa kuondoka gerezani Jumanne wiki ijayo ili kuhudhurie mwenyewe katika kesi ya ufisafi.

Uamuzi huu wa mahakama unakuja zaidi ya wiki moja baaada ya zaidi ya watu 300 kuawa wakati wa maandamano yaliyosababishwa na kukamatwa Zuma kwa kukiuaka agizo la mahakama katika kesi tofauti.

Kua uwezekano wa kupelekwa kwa maafisa wengi wa usalama kwani wafuasi wa Zuma wanatarajiwa kukusanyika katika nje ya mahakama hiyo ya ufisadi katika mji wa Pietermaritzburg - ambao uliathiriwa vibaya na maandamano ya ghasia na uporaji.

Hii itakuwa mara ya pili Zuma kuonekana hadharani tangu alipozuiliwa mwei uliopita.

Wiki iliyopita aliruhusiwa kuhudhuria mazishi ya ndugu yake.

Waendesha mashtaka walikuwa wamependekeza kesi hiyo kuendeshwa kwa njia ya kidijitali - wakitoa sababu za kiusalama.

Lakini jaji ameridhia ombi la Zuma la kuodoka gerezani na kufika mwenyewe katika mahakama ya Pietermaritzburg.

Washirika wa Zuma wameshtuhumiwa kwa kujaribu kuongoza ghasia dhidi ya serikali.

Kesi hiyo inahusiana na makubaliano ya silaha ya miaka ya 1990, na madai kwamba Zuma alipokea hongo. Anakanusha mashtaka yote.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...