Monday, August 9, 2021

Mabinti Wanapimwa Bikra Ndipo Wanajiunga Jeshini




JESHI la Indonesia limedokeza kuwa litakomesha vipimo vya lazima vya "ubikira" kwa makurutu wa kike, katika hatua ambayo imepokelewa vyema na vikundi vya haki za binadamu.



Kwa miongo kadhaa, jeshi limekuwa likiwataka makurutu wa kike kukubali kupimwa ili kujua iwapo ni mabikira au la ,mtindo ambao kundi la kutetea haki za binadamu Human Rights watch limesema ni'udhalilishaji' na 'usiokuwa na msingi wa kisayansi.'



Wakati wa vipimo hivyo , wanawake waliingiziwa vidole viwili katika sehemu zao za siri na daktari wa jinsia yoyote kwa lengo la kujua iwapo walikuwa mabikira au la.





Shirika la Human Rights Watch limesema kitendo hicho ni sawa na "unyanyasaji wa kijinsia."



Upimaji wa ubikira ni kitendo kilichopuuzwa na kulaaniwa ambacho Shirika la Afya Ulimwenguni limesema "halina uhalali wa kisayansi" na ni "ukiukaji wa haki za binadamu za mwathiriwa."

 

Akizungumza katika hotuba iliyowekwa Youtube mwezi jana mkuu wa jeshi ,jenerali Andika Perkasa aliashiria kwamba vipimo vya ubikira sasa vitakomeshwa na badala yake mafunzo yataangazia 'uwezo.'
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...