Mwanariadha wa Kenya, Eliud Kipchoge Jumapili hii ameibuka mshindi wa mbio za marathon kwa wanaume katika michuano ya Olimpiki huko Japan.
Kipchoge amekuwa mwanariadha wa kwanza wa Kenya tangu mwaka 1980 kuuchukua ubingwa wa marathon kwenye olimpiki. Ametumia masaa 2, dakika 8 na sekunde 38 kumaliza mbio hizo na kuwa mkimbiaji wa tatu pekee kuwahi kushinda olimpiki mara mbili.
"Nadhani nimetimiza heshima yangu kwa kushinda marathon kwa mara ya pili, mfululizo. Naamini sasa itasaidia kuhamasisha kizazi kijacho," amesema Kipchoge anayeshikilia rekodi ya dunia. "Ninafurahi kutetea ubingwa wangu na kukikionesha kizazi kijacho, kama utaheshimu mchezo huu na kuwa na nidhamu unaweza kukamilisha kazi yako," ameongeza.
Amefuatiwa na Abdi Nageeye wa Uholanzi aliyekuwa nyuma kwa sekunde 20. Mshindi wa tatu ni Bashir Abdi wa Ubelgiji aliyemshinda Lawrence Cherono wa Kenya.
Read More: Nafasi za Ajira Serikalini na Mashiriki Binafsi Nimekuwekea Hapa
Tanzania imewakilishwa na Alphonce Simbu aliyeshika nafasi ya 7 kwa kutumia masaa mawili, dakika 11 na sekunde 25. Kupitia Instagram, Simbu ameandika, "Asante Mungu, nimemaliza nafasi ya 7 kwenye michezo ya olimpiki nikiwakilisha nchi yangu Tanzania.