Tuesday, July 27, 2021

Mikoa Saba Kuzalisha Hewa Ya Oxijeni


SERIKALI imesimika mitambo ya kuzalisha hewa ya Oxijeni  kwenye mikoa ya Mtwara, Mbeya, Dar es Salaam, Manyara, Songea, Dodoma na Geita.


Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto, Dk Leonard Subi, amesema baada ya zoezi hilo kwa sasa kuna utoshelevu.


Hospitali za rufaa za Mikoa KCMC mjini Moshi na Bugando Mwanza zililalamikia kuzidiwa na wagonjwa wanaohitaji hewa ya Oxijeni hivi karibuni.


KCMC wana mtambo ambao unazalisha hewa ya oxgen kwa siku mitungi 400 .


Dk Subi alisema ni vyema wananchi wakachukua taadhari ya kujikinga na Corona la sivyo mitungi ya Oxijeni haitakaa itoshe.


"KCMC wanazalisha mitungi 400, Arusha pia na Mwanza, tumewaongezea mingjne ili kukabiliana na janga hili, ni vizuri kuchukua taadhari maana mitungi yote ikienda kwenye Corona tunawadhulumu wengine wajawazito wanaojifungua, Watoto na wengine maana inabidi mitungi itolewe kwenye wadi zao wapelekewe wao, kila mtu ajilinde ili  tupunguze kutumia Oxygen," alisema Dk Subi


Aidha Dk Subi,  aliwataka wananchi kuipokea chanjo ya kujikinga na Corona kwa kuwa pindi mgonjwa apatapo akiwa amechanja itaepusha kufikia hatua ya kuhitaji  huduma ya oxygen lakini pia akiendelea na majukumu yake.


Kuhusu ubora wa chanjo na muda uliotumika kuzitengeneza , Profesa Karim Manji, alisema kila mara teknolojia inabadilika, hivyo hata katika utengenezaji wa chanjo yapo mabadiliko makubwa, na chanjo itakayotolewa ni sahihi na imara.


Msisitizo huo unakuja ikiwa kesho saa tatu asubuhi, Rais Samia Suluhu, ataongoza watanzania kupata chanjo ya Corona ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa chanjo hiyo nchini, ambapo pia wakuu wa Mikoni wametakiwa kuongoza uzinduzi huo katika mikoa yao.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...