Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Julai 13, 2021 kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa wa Morocco Nasser Bourita na Waziri Mkuu wa Morocco Saad Dine El Otmani.
Katika Mzungumzo hayo Waziri Mkuu alizungumzia kuimarisha ushirikiano mzuri na wa kihistoria kati ya Tanzania na Morocco ulioasisiwa na kujengwa na wasasisi wa nchi hizi mbili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mfalme Mohammed V.
Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa nchi hizi kuendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Kilimo, Utalii, Nishati na Uvuvi.
Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Leila Muhamed Mussa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.