Wednesday, July 14, 2021

Ali Kiba Amkwepa Diamond Platnumz “Siko Tayari Kuendeleza Bifu na Mtu yeyote"


MKALI wa Bongofleva, Ali Salehe Kiba 'Alikiba' amesema kuwa hayuko tayari kuendeleza chuki na mtu yeyote kuanzia sasa. Akizungumza na kituo kimoja cha redio nchini Kenya, Alikiba ambaye anatamba na ngoma zake mbili kali za Ndombolo na Salute, alisema hataki kuendeleza bifu na mtu iwapo bifu hiyo si ya kibiashara.

"Siko tayari kuendeleza bifu na mtu yeyote, kama hiyo bifu sio ya kibiashara, kwa sababu kuanzisha chuki na mtu huwa inaharibu mambo mengi kama uhusiano," alisema Alikiba.

Licha ya kwamba Alikiba kwa muda mrefu amekuwa akitajwa kuwa katika bifu kali na mkali mwenzie, Diamond Platnumz alisema, "Huwa sifuatilii chuki, na siwezi kubishana na wasanii wenzangu kwa maana hainisaidii kukuza muziki wangu. Huwa nasaidia kila mtu ili naye awe ananisaidia pia au lah, kitu cha muhimu kwangu ni kuwa na ukaribu na mashabiki wangu na kutengeneza muziki mzuri," alisema.

Alikiba aliweka wazi kwamba anajiandaa kutoa albamu yake mwaka huu na mashabiki wanapaswa kuwa tayari kwani itakuwa ya kushangaza.


STORI; MWANDISHI WETU

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...