Kiongozi wa kundi linalotaka kujitenga kwa BiafraNnamdi Kanu anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo jumatatukatika mji mkuu Abuja kujibu mashtaka ya uhaini .
Kundi lake laIndigenous People of Biafra, linalotaka kujitenga kwa jimbo la lao mashariki mwa Nigerialimepigwa marufuku na serikali kuu .
Bw. Kanu aliibuka kama sura mpya ya harakati za kundi hilotakriban miaka 50 tangu kukamilika kwa vita vya Biafra vilivyosababisha vifo vya Zaidi ya watu milioni moja .Alikamatwa na kupelekwa Nigeria mwezi uliopita
