Akiongea wakati zoezi la kuzima moto usiku huo likiendelea, Prof. Mkumbo alisema licha ya Zimamoto kujitahidi kuzima lakini moto ulikuwa mkubwa.
''Moto ni mkubwa sana, wataalam wetu wanaendelea lakini kwakweli moto ni mkubwa. Jengo la soko hili lilikuwa limezungukwa na vifaa vya kuzima moto lakini wafanyabiashara walishaviingilia hivyo havifanyi kazi tena," alisema Prof. Mkumbo.
Aidha aliongeza kuwa baada ya tathmini kufanyika, basi huko mbele wataona namna ya kuwapanga vizuri wafanyabiashara ili kuepusha madhara kama ambayo yamejitokeza usiku wa Julai 10, 2021 wakati soko la Kariakoo likiungua.
Hadi asubuhi ya leo Julai 11, 2021 Bado taarifa zaidi kutoka kwa mamlaka juu ya tathmini ya hasara na athari zilizotokana na moto huo haijatolewa.