Wednesday, May 19, 2021

UN yatangaza kuwa Israel yazuia msaada kufika Gaza

Umoja wa Mataifa (UN) umetangaza kuwa Israel inazuia usafirishaji wa misaada kutoka Lango la Mpaka wa Kerm Abu Salim kwenda Gaza.

Mshauri wa vyombo vya habari wa UN Palestina Adnan Abu Hasna amesema kuwa Israeli imekataa kupeleka misaada ya kibinadamu kwenda Gaza kutoka lango la mpaka wa Kerm Abu Salim, na malori ya misaada yalilazimika kurudi kutoka mpakani.

Abu Hasna pia amesema kuwa mamlaka ya Israeli haikumruhusu Kamishna wa UNRWA kuingia Ukanda wa Gaza.

Mark Lowcock, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu, alisema jana, "Nina wasiwasi sana juu ya ulipuaji wa mabomu wa Israeli wa Gaza. Gaza, ambapo watu milioni 2 wametengwa na ulimwengu kwa nguvu kwa muda muda wa miaka 13, hakuna mahali salama.".

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...