Mgeni rasmi Victor Mkwizu akizungumza kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumla ya wanachuo 92 wakiwemo wasichana 33 na wavulana 59 wamehitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) mwaka 2021 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga.
Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Mei 21,2021 ambapo mgeni rasmi alikuwa Diwani wa Kata ya Ngokolo Mhe. Victor Mkwizu akimwakilisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila.
Akizungumza katika mahafali hayo, Mkwizu amewataka wazazi kupeleka watoto wao katika chuo cha VETA kwani kuna mafunzo ya fani mbalimbali zitakazowawezesha kuajiriwa ama kuajiri wao wenyewe ili kujiinua kiuchumi.
Pia amewasihi vijana hao kuunda vikundi na kujiajiri kupitia mikopo inayotolewa katika Halmashauri za wilaya hivyo wachangamkie fursa ya mikopo ya asilimia 10 (4 vijana, 4 wanawake na 2 watu wenye ulemavu) zinazotengwa na halmashauri za wilaya.
Aidha ameishukuru serikali kwa kuboresha na kujenga vyuo vya ufundi stadi wilayani Kishapu na Igunga mkoani Tabora hali itakayosaidia kupata mafundi wa kutosha na kutanua wigo katika viwanda vinavyojengwa nchini.
Aidha amesema Manispaa ya Shinyanga imeandaa mazingira mazuri katika kuvutia wawekezaji kwenye ujenzi wa viwanda vikubwa, vya kati na vidogo na kutokana na uwepo vyuo vya ufundi vitasaidia kupata mafundi kwa ajili ya viwanda hivyo.
Kuhusu upungufu wa mabweni na madarasa ameshauri chuo kikae na wanajamii , wawekezaji na wadau ili kushirikiana kujenga kwa ajili ya kupunguza adha chuoni hapo.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele amesema kinatoa mafunzo ya Kozi 10 za muda mrefu na kozi fupi zaidi ya 27 na kwamba mpasaa kinahudumia mkoa mzima wa Shinyanga na wana vyuo washirika zaidi ya 10 vya watu binafsi na mashirika ya dini na sasa ujenzi wa Chuo cha VETA Kishapu unaendelea.
Amewaomba wadau wanaoweza kuwekeza katika mabweni wasaidie ili kuondokana na changamoto ya wanafunzi kukaa mtaani.
"Changamoto ya usafiri pia ipo wanachuo wanatumia baiskeli na bodaboda ili kuondokana na changamoto za ajali ambazo zimekuwa zikitokea tunaomba manispaa ya Shinyanga isaidie kupatikana kwa usafiri wa mabasi",amesema Mabelele.
"Bado watu wa Shinyanga hawana muamko wa kuja kupata mafunzo hapa VETA bado ipo. Tunapata wanafunzi kutoka maeneo ya nje ya Shinyanga lakini watoto wa hapa hawataki kuja kusoma hapa, kozi za muda mfupi zipo lakini hawaji",ameongeza.
Ametumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa Shinyanga kutumia chuo cha VETA kupata ujuzi mbalimbali ili wajikwamue kiuchumi, akiwasisitiza viongozi wawahamasishe vijana kupata kupata kozi za muda mfupi na za muda mrefu waone umuhimu wa kuwa na mafunzo ya ufundi stadi.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi, Jackson Shauri amewapongeza vijana hao kwa kuhitimu mafunzo hayo muhimu ya ufundi na kuwasihi kutodharau walichojifunza chuoni kwani wanaweza kuyatumia kujiajiri huku akiwataka wazazi kuachana na mambo ya uswahili hivyo wapeleke vijana wao chuo cha VETA badala ya kuwaacha warande rande mtaani bila kazi.
Akisoma Risala ya Wahitimu Daraja la III VETA Shinyanga mwaka 2021, Judith Mchalo amesema waliohitimu ni 92 kati yao wasichana ni 33 na wavulana 59 ambao wamehitimu mafunzo katika fani mbalimbali ikiwemo Fani ya Umeme,Ubunifu,ushonaji na teknolojia ya nguo,Bomba na ujenzi.
Ameyataja baadhi ya mafanikio waliyopata wakiwa chuoni kuwa ni pamoja na kupata mafunzo ya ufundi stadi,wamepata ujuzi wa kutosha, wameshiriki kazi za ujenzi katika vyuo vya VET Kishapu na Igunga na wanajiamini katika kufanya kazi kwa weledi bila kusimamiwa na mtu yeyote.
Amesema changamoto zilizopo ni upungufu wa vyumba vya madarasa,upungufu wa mabweni kwa ajili ya wanachuo kwani wanachuo wengi wanaishi nje ya chuo hadi kusababisha utoro sugu kwa baadhi ya wanafunzi wa kutwa.
Ameongeza kuwa wanatarajia kukutana na changamoto ya ajira hali inayochangiwa na ukosefu wa mitaji hivyo kuziomba taasisi zinazohusika na mikopo ziweke utaratibu unaoweza kutekelezeka kwa vijana wengi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Jumla ya wanachuo 92 wakiwemo wasichana 33 na wavulana 59 wakiandamana wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumla ya wanachuo 92 wakiwemo wasichana 33 na wavulana 59 wakiandamana wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Jumla ya wanachuo 92 wakiwemo wasichana 33 na wavulana 59 wakiimba wimbo wa chuo cha VETA wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Mgeni rasmi Victor Mkwizu akizungumza kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Mgeni rasmi Victor Mkwizu akizungumza kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Mgeni rasmi Victor Mkwizu akizungumza kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele akizungumza wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.

Mratibu wa Mafunzo VETA Shinyanga, Rashid Ntahigie akizungumza wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Judith Mchalo akisoma Risala ya Wahitimu Daraja la III VETA Shinyanga mwaka 2021, wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021. Kulia ni Abubakari Abdallah.
Mzazi Jackson Shauri akizungumza wakati wa mahafali hayo
Wahitimu Daraja la III VETA Shinyanga mwaka 2021 wakiwa kwenye Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.

Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Vijana wa Kundi la Kambi ya Nyani wakitoa burudani wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya 35 ya kuhitimu elimu ya mafunzo ya ufundi stadi daraja la tatu (III) katika Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga leo Ijumaa Mei 21,2021.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali
Wanafunzi wakiwa kwenye mahafali
Zoezi la kutoa zawadi likiendelea