Saturday, May 15, 2021

Kampeni za ACT sasa bila Chopper


Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kuwa kitafanya mikutano yake ya kampeni katika majimbo ya Buhigwe na Muhambwe kwa kutumia magari baada ya Chopper waliyokuwa  wanaitumia kupata hitilafu.

ACT-Wazalendo  imebainisha hayo kupitia taarifa iliyotolewa leo  na Naibu Katibu Habari, Mawasiliano ya Umma na Uenezi, Janeth Rithe ilieleza kuwa helikopta waliyoikodisha si salama na bado haijafanyiwa matengenezo na hivyo kutokuwa salama kwa matumizi.

Taarifa ya ACT-Wazalendo imeeleza kuwa mikutano yote sita iliyokuwa ifanyike leo katika majimbo hayo, itafanyikia kama awali ilivyopangwa ila kwa kutumia msafara wa magari.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...