Na Maridhia Ngemela
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila alipokuwa akitia hotuba kwa wafanyabiashara ,wakuu wa idara za serikali,wakuu wa wilaya ,kamati ya usalama na ulinzi, katika zoezi la makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amesema machinga wafuate utaratibu wa kufanya biashara zao
Chalamila amesema mkoa huo ni kitovu cha bisahara hivyo anajukum la kukaa na wafanya biashara mkoani hapa ilikuweka mikakati na mbinu za uhamasichaji wa uwekezaji.
Amesema maswala ya kuhusu uwekezaji nikukaa na makundi nakufanya kikao cha wafanya bisahara na wawekezaji katika sekta ya biashara iliwaweze kuelezea serikali inakwama wapi kwani huo ndo muelekeo wa Mh. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu.
Mkuu wa mkoa amewataka machinga kufuata utaratibu sahihi kwakuwasaidia viongozi katika kazi zao kwa kutofanyia bisahara barabarani yanapopita magari yaliyojengwa na tanroad na kwenda kwenye viwanja vya kufanyia biashara.
Amesema lengo la serikali la kuwatoza machinga elfu ishirini ni njia moja wapo ya kuwafundisha kulipa kodi ili anapokuja kuwa mfanyabiashara mkubwa afahamu umuhimu wa kulipa kodi serikalini.
Chalamila amesema katika sekta ya afya wanachi wasitumie vibaya msamaha wa serikali ili kuwapa nafasi wenye uhitaji waweze kupata matibabu kwani serikali inania njema kwa watu wasiojiweza hususani kwa wazee,watoto na mama wajawazito.
Naye mkurugenzi wa Uhuru hospital dk.derick Nyasebwa amesema watu wanajali kununua nguo na kuendekeza starehe wanashindwa kulipia bima ya afya itakayosaidia kuepuka kutumia misamaha na kuacha watu wenye uhitaji wa huduma hiyo.
Nyasebwa amewashauri wananchi kuwekeza katika afya kwani bila afya njema huwezi kufanya kitu ukiwa kitandani .
Kwa ubande wake mfanyabiashara kutoka Birchand group kampuni inayoshughulika na uzalishaji pamba na uuzaji mafuta ya kula Mohamed Ibrahim amesema wako tayalikutoa ushirikiano kwa mkuu wa mkoa Chalamila ilikuweza kufanya maendeleo katika mkoa wa Mwanza.