WAKATIkikosi chake kikitarajiwa kujitupa uwanjani leo, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi atakuwa na wakati mzuri kutokana na asilimia 99 ya wachezaji wake kuwa fiti huku mabadiliko makubwa ya wachezaji yakiwepo.
Yanga inatarajiwa kuvaana na KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa saa moja kamili usiku kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Msimamo unaonyesha kuwa, Yanga wako kileleni wakiwa na alama 50 wakati KMC wako nafasi ya tano wakiwa na alama 35.
Timu hiyo inayoongoza katika msimamo ikiwa na pointi 50, itashuka uwanjani ikiwa na kocha wake Mwambusi ambaye kwa mara ya kwanza ataliongoza benchi hilo.
Mwambusi atakuwa na wakati mzuri kutokana na rundo la wachezaji waliokuwa na majeraha kupona na wapo fiti kwa ajili ya ligi kwa kuanzia mchezo wa leo.Kwa sasa wachezaji watakaokosekana katika mchezo dhidi ya KMC kutokana na matatizo mbalimbali ni Haruna Niyonzima, Yassin Mustapha na Mapinduzi Balama ambaye anafanya programu ya peke yake ya mazoezi binafsi na Carlos Fernandez 'Carlinhos' anayemalizia adhabu ya kadi nyekundu.
Wengine wote wapo fiti akiwemo Said Ntibazokinza 'Saido', Yacouba Songne, Michael Sarpong, Fiston Abdoulrazack na Dickson Job ambaye hajacheza mchezo wowote tangu ajiunge na kikosi hicho kwenye dirisha dogo msimu huu.
Kupona kwa Job kutawapa changamoto mabeki akina Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto ambao wamekuwa chaguo la kwanza kwenye safu ya ulinzi.
Hivyo upo uwezekano mkubwa wa beki huyo kuanza katika kikosi cha kwanza.Lakini pia kurejea kwa Saido ni faida kubwa kwa Mwambusi ambaye yupo kwenye uweze kano mkubwa wa kumtumia nyota huyo wa Burundi katika kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji.
Pia, kiungo fundi Niyonzima alikuwa na wakati mzuri wakati akiitumikia timu ya Taifa ya Rwanda kwani alionyesha kiwango kizuri katika michezo dhidi ya Msumbiji na Cameroon ya kuwania kufuzu Afcon akiwa nahodha.Hivyo upo uwezekano mkubwa wa mabadiliko ya kikosi cha kwanza atakachokitumia Mwambusi katika kuelekea mchezo huo mgumu dhidi ya KMC.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mwambusi alisema: "Ni kweli kesho (leo) tunaanza kucheza mechi zetu zilizobaki, tunaanza na KMC, ni mchezo ambao mimi niliuangalia, tulicheza 'away' (ugenini) tukapata matokeo, wachezaji wangu wamejiandaa vizuri, wamejiandaa kiufundi. Tutacheza bila kukaa nyuma sana, tutacheza mpira wa kushambulia ili kupata matokeo, na tuweze kuwapa Wanayanga kile ambacho wanatarajia kutoka kwenye kikosi chao.
"Akina Lamine na kikosi chao, wahakikishe ndani ya kano mkubwa wa kumtumia nyota huyo wa Burundi katika kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji.
Pia, kiungo fundi Niyonzima alikuwa na wakati mzuri wakati akiitumikia timu ya Taifa ya Rwanda kwani alionyesha kiwango kizuri katika michezo dhidi ya Msumbiji na Cameroon uwanja sasa yale tuliyokuwa tunaambiana kwenye mapumziko na mazoezi tuliyofanya, wanayatumia kesho (leo). Tunajua KMC ni timu nzuri sana, 'especially' (hasa) inapokutana na Yanga, tunalijua hilo.
Hali kama hiyo ndiyo inatukomaza kuonyesha kuwa ni timu kubwa, na timu kubwa lazima udhihirishe ubora wako ndani ya uwanja."Naye, Habib Kondo, Kocha Msaidizi wa KMC, alisema: "Hatuiogopi Yanga kwenye njia zote kwa sababu mpira sio mchezo wa ngumi, tunasema kwamba timu bora haifungwi mara mbili hivyo mbinu zetu zipo vizuri na watatuona ndani ya dakika 90.
" Kwa upande wa KMC, nahodha Juma Kaseja alisema: "Kila mchezaji anahitaji pointi tatu, tunawaheshimu wapinzani wetu kwa sababu ni timu kubwa lakini ndani ya uwanja tutakuwa 11, hivyo tutapambana kusaka pointi tatu."