Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania THRDC umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa agizo lake la kufunguliwa kwa baadhi ya vyombo vya habari vilivyofungiwa.
Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari Mtandao huo umesema huo ni mwanzo wa kuleta matumaini mapya yenye uhai kwa vyombo vya Habari.
Katika kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa na vyombo vya habari huru na vyenye mchango katika maendeleo, Mtandao huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali umekua ukisaidia kwa namna mbalimbali sekta ya habari.